Translation Games: Kiswahili

Màu nền
Font chữ
Font size
Chiều cao dòng

Mkutano wa Chajio

sdvale

Iliyotafsiriwa na Lujayna


Anakuja kutoka kwa nafasi kati ya walimwengu. Ana urembo, mwenye mikono na kujaa nguvu, akiwa anapanda ngazi. Nyumba kimya, usiku mkimya. Harufu iliyotapakaa ni ya binadamu, nyoyo zao hafifu zikipiga damu. Walienda wapi?

Harufu nyengine inamzubaisha kuwinda. Nzuri, inayomchokoza na kumpendeza. Sahani kwenye meza na juu yake—mnyama mwengine mwenye mikono? Mweupe, mwembamba, aliyesokoteka na kufinywa na nyama nyekundu iliyopondwa kama ambaye ni watu walikatwa naye na akaloweka kwenye miili yao.

Hawezi kusoma karatasi iliyoandikwa: Usiku wa Kula Spaghetti.

Furaha inamwingia Mwangamizi. Ama ni hamu ya kumwaga damu? Hasira? La...ni mapenzi.

Bạn đang đọc truyện trên: Truyen2U.Pro